Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Mtwara

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara kuanzia Septemba 14 hadi 17 mwaka huu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas, amesema katika ziara hiyo, Rais Samia atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Aidha, Rais Samia atafuatilia utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kuwa yanatekelezwa.

Kufuatia ziara hiyo, Kanali Abbas, amewaomba wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais mara atakapowasili katika mkoa huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 2021.

Wafuga Nyuki Duniani Kukutana Tanzania

0

Tanzania imetangazwa mshindi wa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Dunia wa Kongresi ya Wafugaji Nyuki (APIMONDIA) ambao huleta pamoja takribani watu 4,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Uamuzi huo umetangazwa nchini Chile unakofanyika mkutano wa mwaka huu wa dunia ambapo Tanzania iliingia raundi ya mwisho na kupambana na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Kamishna Bennedict Wakulyamba, Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili, Dkt. Deusdedit Bwoyo.

Mashujaa Wamerejea

0

Timu ya Taifa ya soka kwa wanaume (Taifa Stars), imewasili nchini leo alfajiri ikitokea Algeria ilipokwenda kucheza mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023.

Katika Kundi F, Tanzania imefuzu pamoja na Algeria ambapo mashindano hayo yatafanyika nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwaka 2024.

COLLABORATION REMAINS THE GUIDING LIGHT FOR ACHIEVING FOOD SECURITY IN AFRICA

0

The Africa Food Systems Forum 2023 has officially concluded today by Deputy Prime Minister Dr. Doto Biteko , underscoring the critical need to expand existing initiatives in order to expedite the transformation of food systems across the continent.

In its 13th Annual Forum, this distinguished platform facilitated comprehensive deliberations among Africa’s foremost intellectual minds, policymakers, and innovators. The focus was on exploring the most recent breakthroughs and best practices within the realms of agriculture and the transformation of food systems.

Eminent speakers at the Forum underscored the importance of visionary thought leadership to hasten the implementation of strategies aimed at translating food system objectives and commitments into tangible actions, particularly with regard to addressing climate change.

Over the course of this four-day Forum, various institutions pledged their commitment to accelerating investments in the youth and women, thereby contributing to a brighter future for Africa.

Hussein Mohamed Bashe, the Minister for Agriculture in Tanzania, unequivocally declared his government’s dedication to placing the youth and women at the epicentre of the Food Systems transformation. He duly acknowledged the pivotal role of the private sector and called for equitable investments.

“In Africa, smallholder farmers do not seek assistance; they demand their rightful and equitable share of global funding,” he asserted.

Amath Pathe, the Managing Director of the Africa Food Systems Forum, extended his gratitude to Dr. Samia Suluhu Hassan, the President of the United Republic of Tanzania, for the remarkable hospitality extended by her government. He emphasised the pivotal role of actions at the national level in revitalizing food systems.

“This year, the Africa Food Systems Forum has hosted the highest number of delegates thus far,” he noted.

The discussions held at the Forum underscored that collaboration remains the guiding force for progress. They reiterated that partnerships among governments, businesses, civil society, farmer organisations, and research institutions will shape a future in which sustainable and prosperous food systems underpin Africa’s advancement.

The Africa Food Systems Forum 2023 witnessed the participation of over 5,400 delegates, including 5 Heads of State and 30 Ministers from 90 countries.

KUANZIA LEO IJULIKANE KAMA AFS FORUM

0

Haiemariam Desalegn, Waziri Mkuu Mtaafu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya AGRF, akitoa pongezi na salamu kwa washiriki wa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 amesema wadhamini wa mkutano huo wameazimia kwa pamoja kubadili jina lake.

Ametangaza rasmi jina la mkutano huo kutoka kuitwa ‘AFRICA GREEN REVOLUTION FORUM’ (AGRF) kwa miaka iliyopita na sasa rasmi kuitwa ‘AFRICA FOOD SYSTEMS FORUM’ (AFS FORUM) likimaanisha Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika.

Ameitaka pia Rwanda kuliweka maanani jina hilo kwa kuwa wanatazamia kuwa na jukwaa la aina hiyo siku za mbeleni.

Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 lililoanza Septemba 5, 2023 limehitimishwa leo na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko

BBT kunufaika na dola milioni 50

0

Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika umekuwa na matokeo chanya kwa upande wa program ya ‘Jenga Kesho Bora’ (BBT) kutokana na benki ya CRDB kwa kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mazingira (GCF) kutoa kiasi cha Dola milioni 50 zitakazotumika katika utekelezaji wa program hiyo.

Hayo yamebainika wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mpango wa kuwezesha wavuvi nchini inayoratibiwa na benki ya CRDB tukio lililofanyika leo na kushuhudiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Ulega amesema kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha vijana hao wanapata mtaji mara baada ya kumaliza mafunzo yao kwa vitendo.

“Hii inamaanisha kuwa hawa wajasiriamali tunaowatengeneza kwa upande wa sekta za Mifugo na Uvuvi sasa wamepata uhakika kabisa wa kupata mikopo yao na kwa kuwa tayari wana maandiko mazuri ya biashara wataingia moja kwa moja kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hizo mbili,” amesema Waziri Ulega.

Ulega ametoa wito kwa benki hiyo kugeukia upande wa tasnia ya ufugaji wa samaki ambako ameweka wazi kuwa anaamini kuna faida kubwa endapo wafugaji hao watawezeshwa rasilimali fedha na zana mbalimbali za kisasa za kufanyia shughuli hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, AbdulMajid Nsekela amesema mikopo yenye masharti nafuu itawapa fursa vijana hao kujipanga kwani ina muda mrefu zaidi wa matazamio kuliko aina nyingine zote za mikopo inayotolewa na benki hiyo.

TTCL kuunganisha mataifa ya afrika

0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha linaendelea kutoa huduma bora za mawasiliano ili kurahisisha shughuli za maendeleo na kuunganisha mataifa ya Afrika katika masuala ya mawasiliano na mtandao.

Hayo yamebainishwa leo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya kuunganisha mkongo wa taifa wa mawasiliano wa NICTBB na mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na ESCOM- Malawi ambao umeshuhudiwa na mawaziri kutoka
wizara zinazohusika na mawasiliano nchini Tanzania na Malawi hafla iliyofanyika mjini Unguja.

Aidha, Waziri Nape amesema mkataba huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu katika nchi za Afrika ikiwemo ziara yake nchini Malawi iliyozaa mkataba huo wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili.