Wafuga Nyuki Duniani Kukutana Tanzania

0
150

Tanzania imetangazwa mshindi wa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Dunia wa Kongresi ya Wafugaji Nyuki (APIMONDIA) ambao huleta pamoja takribani watu 4,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Uamuzi huo umetangazwa nchini Chile unakofanyika mkutano wa mwaka huu wa dunia ambapo Tanzania iliingia raundi ya mwisho na kupambana na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Kamishna Bennedict Wakulyamba, Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili, Dkt. Deusdedit Bwoyo.