Waziri Mkuu wa Cape Verde : Rushwa isiwe kikwazo Afrika

0
178

Waziri Mkuu wa Cape Verde Dkt. Olavo Avelino Garcia Correia amewataka Viongozi wa Afrika kuipiga vita rushwa katika nchini zao.

Dkt. Correia amesema moja kati ya changamoto kubwa Afrika ni rushwa, ambayo imekuwa ikikwamisha upatikanaji wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati na elimu kwa Wananchi wa Bara hilo.

Amesema ili kufikia malengo yanayowekwa na Viongozi wa Afrika wanaokutana Dar es Salaam katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Afrika inapaswa kuongeza mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kubadilisha fikra na baadhi ya mitazamo ya watu wake.

Dkt. Correia
ameonesha kusikitishwa na tabia ya baadhi ya Vijana Barani Afrika kwenda kutafuta fursa nje ya bara hilo kwa kudhani kuwa Afrika hazipo na hivyo kuwataka Viongozi wa Afrika wachukue jambo hilo kama ni changamoto na kutafuta utatuzi wake.