Watu 9 wafariki Ziwa Tanganyika baada ya boti kuzama

0
439

Watu tisa wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika, Mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi, Martin Ottieno amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Rasini.

Kamanda Ottieno ameongeza kuwa boti hiyo iitwayo MV Nzeimana hufanya safari zake kati ya Kijiji cha Sibwesa na Ikola na imezama ikiwa abiria 60, ambapo abiria 51 wameokolewa.

Aidha, amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliosababisha boti hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka.