Watanzania dumisheni amani : Waziri Mkuu

0
249

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akitoa salamu kwa Waumini wa dini ya Kiislam, aliposhiriki Sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge.

“Waislam wenzangu pamoja na jamii nzima hatuna budi kuendelea kutunza amani iliyopo kwa maombi hasa kuwaombea Viongozi wetu wa Kitaifa kuongoza nchi kwa hekima na busara”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Ameongezea kuwa, dini zina mchango mkubwa katika kuimarisha uwepo wa amani, ambayo inatoa fursa kwa jamii kushiriki vema kwenye shughuli za uzalishaji mali za kila siku, hivyo jamii haina budi kuzingatia yale wanayofundishwa katika dini zao ili kudumisha umoja, mshikamano na upendo.