Wananchi washauriwa kutumia Serengeti Safari Marathon kiuchumi

0
115

Wananchi wanaoishi Kanda ya Ziwa wametakiwa kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na mbio za Serengeti Safari Marathon zinazofanyika kila mwaka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ameyasema hayo leo wakati wa kuhitimisha mbio za Serengeti Safari Marathon 2022  katika eneo la Geti  Ndabaka Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

“Tunataka fursa zisambae ili kila mmoja aone umuhimu wa hifadhi hii,” Masanja amesisitiza huku akiwataka kuandaa mazingira mazuri ya kuvutia watalii wanaokuja nchini hasa kutokana na hamasa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour.

Amewaasa waandaaji na washiriki wa mbio hizo kutokata tamaa bali kujenga mshikamano utakaofanikisha ipasavyo mashindano hayo ili kumuunga mkono Mhe.Rais katika kampeni ya Kutangaza Utalii na uwekezaji kupitia Royal Tour.

Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Halfan Haule ambaye pia ni Mkuu Wilaya ya Musoma amewataka washiriki wa mbio hizo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio vilivyoko ndani yake