Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda, amezindua ujenzi wa barabara ya Makongo Juu kwa kiwango cha lami na kusema kuwa, ujenzi huo utakamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Ujenzi wa barabara hiyo ya Makongo Juu yenye urefu wa Kilomita 4.5, utagharimu Shilingi Bilioni 8.9, fedha ambazo zinajumuisha malipo ya fidia pamoja na uhamishaji wa miundombinu ya maji na umeme.
Makonda pia amezindua ujenzi wa barabara ya Madale yenye urefu wa Kilomita Sita, ujenzi utakaofanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na Nusu.