Trump kuwania tena urais

0
114

Aliyekuwa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwania kwa mara nyingine nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2024.

Trump ametangaza kuwa atawania tena kiti hicho ili aliongoze Taifa hilo kwa mara ya pili.

“Ili kuitukuza na kuipa ukuu tena Marekani, leo usiku ninatangaza nia yangu ya kuwa Rais wa Marekani.” amesema Trump

Aidha, Trump ambaye anatoka chama cha Republican
amedai kuwa, chama hicho hakiwezi kuteua mwanasiasa au mgombea wa kawaida endapo kinataka kupeleka Rais Ikulu.

Trump amekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2021.