TAMISEMI NA ZIMAMOTO RAHISI KUFANYA KAZI PAMOJA

0
178

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Eliezer Feleshi ameeleza namna ambavyo Jeshi la Wananchi linashika hatamu pale ambapo majeshi mengine yamekomea huku akifafanua namna ambavyo imeonekana ni vyema Jeshi la Zimamoto kuhushishwa na Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kama ilivyopendekezwa na Tume ya Haki Jinai.

Akizungumza na wahariri wa Vyombo vya habari katika kikao kinachohusu ripoti ya Tume ya Haki Jinai kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Feleshi amesema kuwa kuwepo kwa majeshi mengi ni suala la kikatiba kwani katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampatia mamlaka Rais wa nchi kuanzisha majeshi na pia katiba hiyo inaelekeza dhumuni la kuanzisha majeshi hayo ambapo lazima yaendane na misingi ya kikatiba.

Amefafanua kuwa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai juu ya Jeshi la Zimamoto ni kwa sababu shughuli zake ni za uokoaji hivyo ni vizuri lihusianishwe na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo itakuwa rahisi kuweka mipango yake ambayo imeonekana kuendana zaidi na namna TAMISEMI inapangilia nyenzo na rasilimali zinazoendana na mipango ya matumizi ya ardhi na makazi ya watu na mali nyingine kwani Jieshi hilo linapowekwa mbali na TAMISEMI inashindwa kukaa kwenye vikao vya ngazi ya chini katika mikoa na wilaya.

Vilevile Feleshi ameeleza ni wapi sheria inaruhusu Jeshi la Wananchi kujihusisha na raia, mfano panapotokea tatizo kubwa katika nchi, kutokea jambo ambalo litamhitaji Amiri Jeshi Mkuu kutoa Amri kwa Jeshi hilo kushiriki.