Taarifa ya msemaji mkuu wa serikali

0
256

Serikali imesema itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na vyombo vya habari katika kuhabarisha umma juu ya mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali yao ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya wanchi.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati wa mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam akiwasilisha taarifa ya Serikali juu ya masuala mbalimbali yanayotekelezwa.

“Serikali inawahakikishia kuwa ipo bega kwa bega na nyie wanahabari kutokana na kazi kubwa mnayofanya ya kuhabarisha umma wa Watanzania juu ya mambo yanayotekelezwa na Serikali yao,” amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amebainisha kuwa Serikali imetekeleza ahadi zake ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya reli ya kisasa (SGR), barabara na vituo mbalimbali za afya nchini.

Pia amesema serikali imeanza kulipa mishahara ya Wafanyakazi kwa wakati ikiwemo mishahara ya madiwani ambayo inatolewa na Serikali kupitia hazina, ambapo zaidi ya bilioni 600 zimetolewa na Serikali.

Kuhusu chanjo ya UVIKO-19 ambayo imeanza kutolewa nchini baada kuzinduliwa siku chache zilizopita na Rais Samia Suluhu Hassan, amesema chanjo hiyo ni hiari na kwamba Serikali haijamlazimisha mtu yeyote hivyo kuwataka wananchi.

“Serikali imeanza kutoa chanjo hiyo kwa ajili ya makundi maalumu wakiwemo madaktari, wazee na watu wenye matatizo ya afya,” amesisitiza Msigwa.

Kuhusu tozo za miamala ya simu amebainisha kuwa Serikali kwa kushirikana na wadua wa maendeleo wamepitisha tozo hizo kwa ajili ya kukusanya mapato yatakayotumika kutatua kero za wananchi ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama kupitia makusanyo yatakayopatikana kwenye tozo hizo.