Rais Mwinyi ateua viongozi mbalimbali

0
144

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa makatibu wakuu sita, baadhi wamebadilishwa wizara na wengine wamepandishwa vyeo.

Pia amemteua Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena Said imesema, miongoni mwa walioteuliwa ni Dkt. Islam Seif Salum ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Mwingine aliyeteuliwa na Dkt. Mwinyi ni Thabit Idarous Faina, ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Viongozi wote walioteuliwa wataapishwa kesho Novemba 11, Ikulu jijini Zanzibar.