Rais ateua Mkurugenzi Mkuu Tanesco

0
214

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco.

Kabla ya uteuzi huo Issa alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi (PDB).

Pia amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, kabla ya uteuzi huo Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magahribi wa Multichoice Afrika, Chande anachukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka.