Rais ataka ushirikiano wa vyama vya siasa na vyombo vya habari

0
318

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuboreshwa kwa uhusiano baina ya vyama vya siasa na vyombo vya habari.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo Ikulu mkoani Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu demokrasi ya vyama vingi vya siasa, kikosi chenye wajumbe 25.

Amesema wakati umefika kwa vyama vya siasa na vyombo vya habari kuwa na uhusiano wa karibu muda wote na sio kuwa na migogoro kama ilivyo’zoeleka.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amevitaka vyombo vya habari kutoegemea upande mmoja na kuvitaka kutoandika mabaya tu ya vyama hivyo bali viandike pia mazuri yanayofanywa na vyama hivyo.