Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza Prince Philip, ametoka hospitilini alikokuwa amelazwa kwa muda wa siku nne kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo matabibu wanaompatia tiba kutoka hospitali ya King Edward wamesema licha ya afya yake kuimarika, bado anahitaji uangalizi wa madaktari kuangalia afya yake.