Naibu Waziri Gekul aitaka BASATA kulinda maadili kwa wasanii

0
123

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amefanya ziara katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), taasisi ambazo zipo chini ya wizara hiyo. 

Wakati wa ziara hiyo mkoani Dar es salaam, Naibu Waziri Gekul ametoa maelekezo kwa BASATA kukamilisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa wasanii wote nchini, na pia ameliagiza baraza hilo kusimamia maadili ya Wasanii ipasavyo.

Naibu Waziri Gekul pia ameiagiza BASATA kufufua muziki  wa asili wa Watanzania na kutoa mafunzo kwa Wasanii mara kwa mara.

Akiwa katika
Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Naibu Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amewataka Watendaji wake kuendelea kuchapa kazi, licha ya changamoto kadhaa zinazowakabili.