Mabadiliko ya Njia utakapopita mwili wa Dkt.Magufuli

0
226

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge ametangaza mabadiliko ya njia ambazo mwili wa Marehemu Dkt. John Magufuli utapita mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kuuombea katika kanisa la Mtakatifu Petro.

Akitangaza mabadiliko ya njia hizo, Mkuu wa Mkoa amesema mabadiliko hayo yana lengo la kutoa nafasi kwa wananchi kumuaga aliyekuwa Rais wao Mpendwa Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa ametaja njia ambazo mwili wa Hayati Magufuli utapita ni pamoja na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi mapaka Morocco na kisha msafara huo utakunja kona kupita barabara ya Kawawa mapa magomeni hadi Mzunguko wa Kigogo.

Baada ya hapo Mwili wa Dkt. Magufuli utanyoosha mapaka Katika makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru na kunyoosha mpaka makutano ya barabara ya Nyerere, Changombe na Kawawa na kisha kuelekea uwanja wa Uhuru.

Kunenge amewataka wananchi kujitokeza katika barabara hizo ili kutoa heshima kwa Marehemu Dkt. Magufuli ambaye amelitumikia Taifa kwa upendo mkubwa.

Shughuli za kuuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli zitaanza kesho Machi 20 na mwili wa kiongozi huyo utazikwa Machi 25,2021 Wilayani Chato, Mkoani Geita.