Kiwanda kingine cha Barakoa chazinduliwa

0
118

Serikali kupitia wizara ya Afya imezindua kiwanda kingine cha kutengeneza Barakoa aina ya N95, zinazosaidia kujikinga na magonjwa ya hewa katika maeneo ya kutolea huduma.

Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel aliyemwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika Bohari ya Dawa (MSD) mkoani Dar es Salaam.

“Nimekuja hapa na Balozi wa Japan kuzindua kiwanda cha Barakoa aina ya N95, ukiacha vile vingine vinavyozalisha Barakoa za kawaida, kwa kuzalisha Barakoa hizi kutasaidia katika maeneo ya utoaji huduma na kukuza uchumi wetu kwa kuziuza kwa nchi ambazo hazina uzalishaji huu.” amesema Dkt. Mollel

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Yashushi Misawa ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hasa katika upatikanaji wa vifaa tiba vitakavyosaidia katika matibabu.