Kigoma: Ukuta wa bandari uliogharimu bilioni 2 kubomolewa

0
496

Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma imeitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kubomoa mara moja ukuta wa Bandari Kavu ya Katosho.

Agizo hilo limetolewa kutokana na ukuta wa bandari hiyo kujengwa bila kibali cha mamlaka husika.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameitaka TPA kukaa na manispaa wamelize sintofahamu hiyo.

Ujenzi wa ukuta huo uliokamilika mwezi Disemba 2019 umegharimu shilingi bilioni 2.4.