Jeshi la Lebanon limeingia katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi
hiyo Beirut, – kuanza kutoa vizuizi vya barabarani vilivyokuwa vimewekwa na Waandamanaji na kutatiza usafiri wa barabara.
Waandamanaji nchini Lebanon wamerejea katika mitaa ya mji wa Beirut
kuendelea na maandamano yao ya kupinga Serikali, licha ya Waziri Mkuu
wa nchi hiyo Rafiq Hariri kuachia madaraka, kama walivyokuwa wakidai.
Baadhi ya askari wameonekana wakipambana na Waandamanaji ambao
walikuwa hawana muelekeo wa kusitisha maandamano yao, kwa madai kuwa hawajaridhika na mabadiliko Serikalini.