Wakazi wanaoishi jirani na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameishukuru Serikali kwa kudhibiti wanyama wakali na waharibifu.
Pia wameishukuru Seriikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuboresfa hifadhi hiyo, jambo linalovutia Watalii wengi wanaotembelea hifadhi hiyo.
Josephat Mwenda, ambaye ni mmoja wa Wakazi wa Mang’ula amesema kwa sasa wananufaika na hifadhi kutokana na wageni wengi wanaotembelea Hifadhi hiyo ya Taifa ya Milima ya Udzungwa.
Naye Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ambaye pia ni msimamizi wa mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) Joel Mrema amesema, kupitia mradi huo wamefanikiwa kupata vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja magari.