Dunstan Kyobya ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

0
460
[Picha: Maktaba]

Rais John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Delphine Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

Dkt. Magere anachukua nafasi ya Theresia Mmbando ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Magere alikuwa Ofisi ya Rais akishughulikia masuala ya uchumi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Dunstan Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.

Kyobya anachukua nafasi ya Bw. Evod Mmanda aliyefariki Dunia tarehe 27 Aprili, 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Kyobya alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo  tarehe 06 Mei, 2020.