Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameiagiza wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na wizara ya Maji kuhakikisha pale inapojengwa miradi ya maji iwekwe pia miundombinu ya huduma za Zimamoto.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa jengo la kituo kikuu cha Zimamoto na Uokoaji lililopo Temeke.
Ameongeza kuwa miji inazidi kukua, hivyo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji liendelee kubuni mbinu mbalimbali za utendaji kazi.
Aidha, Makamu wa Rais ameiagiza wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na viongozi wa mikoa mbalimbali katika kutenga maeneo ya ujenzi wa vituo vya Zimamoto na Uokoaji.
Kwa upande wa Serikali Makamu wa Rais amesema, itaendela kufanya jitihada za kutafuta fedha za kuliwezesha jeshi hilo ili liweze kutoa huduma bora kwa Wananchi.