Dkt. Mohamed bosi mpya NECTA

0
173

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Said Ally Mohamed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mohamed alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundishaji, Mafunzo na Mitihani, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Uteuzi huo umeanza Februari 23, 2023.