BASI LA SIMBA LIMEUZWA

0
256

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ambaye anamaliza muda wake na anawania nafasi hiyo kwa muhula wa pili, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kana inavyoelezwa.

Simba ambayo ni muda sasa basi lao limekuwa halionekani huku wakitumia basi dogo ‘Coaster’ na taarifa ya awali ikithibitisha kuwa basi ni bovu sasa imethibitika kwa limeuzwa.

“Nashushiwa lawama ambazo sio zangu, basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi, sikuwa mjumbe wa bodi wala mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,” amesema.

Ameongeza kuwa “lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata utaratibu,” amesema kiongozi huyo.

Uchaguzi wa viongozi wapya wa Simba SC unatarajiwa kufanyika Januari 29 mwaka huu.

Credit : Mwanaspoti