Arsenal kuumana dhidi ya Chelsea boxing day

0
291

Usiku wa boxing day Decemba 26 utakuwa ni usiku wa patashika kwa vijana wa Arsenal ambao wataikaribisha Chelsea katika mchezo wa ligi kuu England, je Arsenal watafungua zawadi zao siku hiyo kwa furaha au maumivu yataendelea baada ya kuchezea vichapo mfululizo katika matokeo ya hivi karibuni?

Manchester City watakipiga dhidi ya Newcastle united , wakati mashetani wekundu Manchester united watachuana na Leicester city katika dimba la king power, Aston Villa dhidi ya Crystal palace wakati Fulham wakiumana vilivyo dhidi ya Southampton na Sheffeld united wakicheza na Everton

Tarehe 27 ya Desemba Liverpool vinara wa ligi hiyo watachuana dhidi ya West Bromwich Albion katika uwanja wa Anfield, Wolverhampton wanderers wakiwakaribisha Tottenham Hotspurs, Leeds United wakicheza dhidi ya Burnley huku West Ham united wakiimaliza weekend kwa mchezo wao dhidi ya Brighton & Hove albion