Ajali ya ndege yaua watalii wa familia moja

0
228

Watalii wanne wa familia moja raia wa Ujerumani pamoja na rubani raia wa Afrika Kusini wamefariki dunia nchini Namibia, baada ndege waliokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.

Polisi nchini Namibia wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya ndege ndogo ya kukodi aina ya Cessna 210, yenye namba za usajili V5 – LMK.

Ndege hiyo ilikuwa inapaa kutoka katika kiwanja cha ndege cha Impalila, Kavango katika hifadhi ya Zambezi.