Vituo vya Polisi Kizimkazi, Makunduchi vyapata magari

0

Vituo vya Polisi kizimkazi na Makunduchi vilivyopo wilaya ya Kusini Unguja vimepatiwa magari kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya usalama.

Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi magari hayo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuzindua miradi ya maendeleo kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

Akihutubia mara baada ya kukabidhi magari hayo Rais Samia amesema, yatawasaidia Askari kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

M Mama kujenga hospitali ya mfano Zanzibar

0

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango wa M Mama unaoratibiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom utajenga hospitali ya mfano visiwani Zanzibar, ili kusaidia Wajawazito kupata huduma kwa wakati.

Akizindua kituo cha afya Kizimkazi kilichojengwa na Vodacom pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)
Rais Samia amesema, mpango huo wa M Mama una manufaa makubwa kwa Wajawazito nchini.

Mbali na kuzindua na kutembelea kituo hicho, Rais Samia pia amezindua gari maalum litakalotumiwa na wataalam wa afya kutekeleza majukumu yao.

Milioni 500 kujenga soko la samaki Kizimkazi

0

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua ujenzi wa soko la kisasa la Samaki katika eneo la Kizimkazi, ambapo wavuvi wa eneo hilo watapata fursa ya kuuza bidhaa zao kiurahisi.

Mrad huo unafadhiliwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 500 na unatarajiwa kuwahudumia wavuvi na wafanyabiashara wa mazao ya samaki wa eneo la kizimkazi na wilaya nzima ya Kusini Unguja.

Rais Samia amesema, Serikali itashirikiana na benki ya CRDB kuhakikisha miundombinu yote muhimu katika soko hilo inawekwa kwa wakati.

Bil 1 kujenga viwanja vya kuchezea Watoto

0

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi ujenzi wa viwanja vya kuchezea Watoto vyenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwenye eneo la kizimkazi wilaya ya Kusini Unguja.

Viwanja hivyo vinajengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB na ujenzi huo utatakamilika baada ya miezi 12.

Akizungumzia mradi huo Rais Samia amesema, ni hatua kubwa kwa wakazi wa Kizimkazi na wilaya nzima ya Kusini Unguja na utatoa fursa kwa watoto kupata fursa ya kujifunza michezo mbalimbali.

Amewataka wadau zaidi kujitokeza kuwekeza katika eneo hilo, kwani fursa bado ipo.

Spika: Kuhusu bandari Bunge limemaliza mjadala

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema
Bunge lina mipaka katika kujadili suala la uwekezaji wa bandari na liliishamaliza mjadala huo, hivyo wanachotakiwa kufanya hivi sasa Wabunge ni kuendelea kuwasikiliza Wananchi.

Dkt. Tulia ameweka wazi kuwa Bunge linawakilisha Wananchi na kuishauri Serikali, hivyo kama litaletewa mkataba wa bandari kwa utaratibu mwingine wa kibunge itakuwa ruksa kwa Wabunge kuchangia.

“Waheshimiwa Wabunge tulienda majimboni tumewasikia Wananchi, lakini pia tumewasikia wale wasio wa majimbo yetu wakiendelea kutoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Uwekezaji bandari sisi kama Wabunge ni kazi yetu kuendelea kuwasikiliza Wananchi na kuisimamia Serikali.” amesema Dkt. Tulia

Spika Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Agosti 29,2023 mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

Wakulima wa chai kunufaika na mkutano wa AGRF

0

Mkurugenzi wa Huduma na Usimamizi kutoka @wizara_ya_kilimo Kemilembe kafanabo ametoa wito kwa Wakulima wa zao la chai nchini kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF)
ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni mkoani Dar es Salaam.

Kemilembe amewasisitiza Wakulima kuchangamkia fursa hiyo kwani watapata taarifa mbalimbali kuhusu soko la zao la chai.

“Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food System Forum) unaleta shauku na hamasa kubwa kwa wazalishaji na wauzaji wa chai kupata taarifa mbalimbali zitakazochochea zao hilo kupata mapato zaidi,” amesema Kemilembe

Pia ametoa wito kwa Wakulima wa chai nchini kuzingatia uzalishaji wa chai unaokidhi viwango na ubora wa Kimataifa, ili kukuza soko la bidhaa hiyo.

Aidha, Mkurugenzi huyo wa Huduma na Usimamizi kutoka @wizara_ya_kilimo amesema vipaumbele vya vya sasa vya kuchochea uzalishaji na mauzo ya zao la chai ni pamoja na kuhamasisha, kusimamia na kudhibiti uzalishaji ili kuongeza ubora wa chai unaokidhi viwango vya soko Kimataifa.

Kwa mujibu wa takwimu za @wizara_ya_kilimo,uzalishaji wa zao la chai umeongezeka kutoka tani elfu 24.8 mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani elfu 26.75 kwa mwaka 2022/2023 ambapo jumla ya tani elfu 21.09 zimeuzwa nje ya nchi.

Madarasa mapya yazinduliwa Kusini Unguja

0

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua vyumba sita vya madarasa katika shule ya msingi Muyuni, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kuzindua miradi ya maendeleo kuelekea kilele cha Tamasha la watu wa Kizimkazi.

Mbali na vyumba hivyo vya madarasa, Rais Samia pia amezindua darasa kwa ajili ya mitihani na ukumbi wa Jumuiya ya watu wa Muyuni kwenye shule ya sekondari ya Muyuni wilaya ya Kusini Unguja.

Akizungumza mara baada ya kuzindua miradi hiyo Rais Samia amesema anajisikia faraja kuona anachangia maendeleo ya mahali alipozaliwa miaka 63 iliyopita.

Amewataka Wananchi wa Muyuni kutunza miundombinu hiyo ili iwasaidie kwa muda mrefu.

WFP yawashika bega wakulima

0

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeipatia wizara ya Kilimo ndege nyuki (drone) na vishkwambi 370 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo nchini.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema vifaa hivyo vitasaidia kukabiliana na uharibifu wa mazao shambani na kusaidia kilimo kuwa na tija katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema ndege nyuki aliyopokea ina uwezo wa kupulizia dawa na viuatilifu katika hekta 20 huku vishkwambi 370 vyenye thamani ya
shilingi Milioni 364 vitarahisisha utekelezaji wa dhana ya kilimo ni sayansi kwa kutatua changamoto za Wakulima kupitia teknolojia.

“Nawashukuru sana WFP kwa kutupatia vifaa hivi, ambapo vishkwambi vinakwenda kugawiwa kwa Maafisa Ugani kwa ajili ya kukusanya taarifa mbalimbali za Kilimo,” amesema Waziri Bashe.

Ameeleza kuwa vifaa hivyo vitaanza kutumika kwa kupima mashamba ya vijana wa programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT).

Naye Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gibson ameeleza kufurahishwa na ushirikiano aliopewa na wizara ya Kilimo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania ili kukuza sekta ya kilimo.