VITUO VYA POLISI KUJENGWA KWA MICHANGO YA WANANCHI

0

Rais Samia suluhu Hassan amesema anatambua mafanikio yanayopatikana kupitia Jeshi la Polisi kwa Wananchi hasa utaratibu wa Polisi Kata, hivyo amemuelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuwa na mkakati wa kuzishirikiaha halmashauri kujua wajibu wao katika kufanikisha ujenzi wa vituo vya Polisi vya kata.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika mkoani Dar es Salaam.

Amesema ikiwa Wananchi watashirikishwa katika upatikanaji wa vituo vya Polisi vya kata, itarahisishwa zaidi upatikanaji wake kuliko kuiachia wizara kubeba jukumu hilo peke yake.

Rais Samia ameongeza kuwa ikiwa Wananchi watashirikishwa na kuona ipo haja wanaweza kufanya peke yao, akitoa mfano wa Kizimkazi, Zanzibar ambapo kulikuwa na uhitaji wa muda mrefu wa kituo cha Polisi ila baada ya Wananchi kushirikishwa kituo hicho kimejengwa na hivi karibuni gari limekabidhiwa kwa kituo hicho ili kusaidia majukumu yake.

KAMERA KUPUNGUZA UHITAJI WA ASKARI BARABARANI

0

ais Samia Suluhu Hassan amesema kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Serikali inakwenda kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Nchini ambapo kamera zitatumika katika maboresho hayo.

Rais Samia ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi.

Ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa magari mabovu yanayotembea barabarani, Jeshi la Polisi linakuja na mfumo wa ukaguzi wa lazima wa magari ambapo kila gari litatakiwa kukaguliwa.

Aidha, Rais Samia amesema Jeshi la Polisi litakuwa na mfumo wa utambuzi wa uchakataji wa taarifa za uhalifu ambao utasaidia kutambua mhalifu kwa njia ya picha, hivyo kulirahisishia jeshi hilo kufanya uchakataji wa taarifa za wahalifu.

Wanaojitolea wapewe kipaumbele Utumishi

0

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameishauri Serikali kuweka utaratibu wa dharura wa kuwapa kipaumbele Wafanyakazi wa kujitolea kwenye suala la ajira wakati mchakato wa sheria ya Wafanyakazi wa kujitolea ukiendelea kuchakatwa.

“Katika kipindi hiki cha kusubiri wakati Serikali mkijipanga maadam wapo, hizo kada mbalimbali za watu wanaojitolea mtafute utaratibu wa muda ama wa mpito wa kuwatazama wakati mnasubiri kufanya marekebisho makubwa kwa sababu wapo na wanaendelea kujitolea.” Ameshauri Spika Tulia

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma katika mkutano wa 12 kikao cha tano Septemba 04, 2023 baada ya Mbunge wa Kiteto, Edward Ole Lekaita kumuuliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ni lini Serikali itapeleka marekebisho ya Sheria ya Ajira ya Utumishi wa Umma kuongeza kigezo cha kujitolea ili kutoa fursa kwa wanaojitolea.

Bunge

Tanzania

Utumishi

Spika

TEHAMA kuwa mjadala mkuu Mkutano wa Jeshi la Polisi

0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema dhima ya mkutano uliozinduliwa hii leo na Rais Samia Suluhu Hassan ni TEHAMA, ikilenga kuimarisha uwazi na uwajibikaji.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Polisi, Waziri Masauni amesema mbali na Jeshi hilo kuibua mifumo ya TEHAMA 13 ili kuongeza ufanisi katika majukumu ya Jeshi hilo ili kuepusha changamoto na kero kwa Wananchi, matumizi ya mifumo hiyo hayaepukiki.

Hata hivyo Masauni ameongeza kuwa kutokana na umuhimu huo, ajira zilizotolewa za Jeshi la Polisi zimetumika kupata askari wa Jeshi hilo wenye taaluma ya TEHAMA takribani 80 ili wasimamie mifumo hiyo.

Waziri Masauni ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Nchini linaendelea kushirikiana na Mashirika ya uzalishaji Mali ambapo Jeshi hilo hivi sasa limefanikiwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kuibua miradi kadhaa.

Ametaja moja ya miradi hiyo kuwa ni ule wa Miji Salama ambao utaanza siku za usoni na kwamba hadi sasa kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwa sio nchi chache basi huenda mradi huo ukawa unapatikana hapa nchini pekee.

POLISI KUIMARISHA USALAMA UCHAGUZI WA 2024, 2025

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Camillus Wambura amesema, Jeshi hilo limekwishaanza maandalizi ya kuimarisha ulinzi na kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

IGP Wambura ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini.

Amesema katika mkutano unaozinduliwa hii leo wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, moja ya mikakati na mipango itakayojadiliwa ni pamoja na hilo la ulinzi na usalama wakati wa chaguzi hizo.

Aidha, IGP Wambura amesema Jeshi la Polisi nchini linaendelea kuhakikisha kunakuwa na usalama katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili kudhibiti wizi wa vifaa pamoja na hujuma.

DAR na mkakati wa ujenzi wa vituo vya Polisi

0

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo umejipanga kujenga vituo vya polisi ili kutoa suluhu ya upungufu wa vituo hivyo kwa mkoa huo.

Kwa sasa Dar es Salaam ina vituo 128 vya polisi ambapo uhitaji ni 217, hivyo kusababisha upungufu wa vituo 89.

Chalamila amesema mkoa wa Dar es Salaam umejipanga kujenga vituo hivyo pungufu ambapo kila halmashauri itajenga vituo viwili ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024.

NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AKIWASILI BUNGENI

0

Picha mbalimbali zikimuonesha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alipokuwa akiwasili Bungeni jijini Dodoma kushiriki kikao cha tano, mkutano wa 12, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kushika wadhifa huo.

https://www.youtube.com/watch?v=NHlZ4Y0umlw