Waandishi wa habari Myanmar wahukumiwa kifungo jela

0

Mahakama nchini Myanmar imewahukumu waandishi wa habari wawili wa shirika la habari la Reuters kifungo cha miaka Saba jela kila mmoja kwa kosa la kufanya uchunguzi wa siri nchini humo kuhusu mgogoro wa Rohingya.

Waandishi hao ambao ni Wa Lone na Kyaw Soe Oo walishitakiwa kwa kosa la kuwa na nyaraka za serikali ambazo walidai kupatiwa na askari polisi, jambo ambalo wamedai lilikuwa limepangwa.

Kesi hiyo imeonekana kwa wengi kuwa ni ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini Myanmar.

Waandishi hao walikuwa wanatafuta ushahidi juu ya mauaji wa wanaume Kumi yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika kijiji cha Inn Din In mwezi September mwaka 2017.

Rais Xi Jinping afungua mkutano wa FOCAC

0

Rais Xi Jinping wa China amefungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Akifungua mkutano huo Rais Xi Jinping amesema kuwa China itatoa Dola Bilioni 60 za Kimarekani kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na Afrika katika shughuli za maendeleo.

Rais Xi Jinping ameahidi kuwa China itatoa ushirikiano ili kuhakikisha kwamba amani ya kudumu inapatikana Barani Afrika, hatua ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Maeneo mengine ambayo Rais huyo wa China ameahidi kuwa nchi yake italisaidia Bara la Afrika ni ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya biashara na huduma za afya.

Kadhalika Rais Xi Jinping amesema kuwa China itatoa nafasi za mafunzo ya kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaam kutoka nchi za Afrika ili kuchangia katika

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo alipata nafasi ya kusalimiana na Rais Xi Jinping baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Ubadhirifu Kampuni ya Huduma za Meli wamkera Rais

0

Rais John Magufuli ameeleza kukerwa na ubadhirifu uliokua ukifanyika katika Kampuni ya Huduma za Meli nchini.

Amesema kuwa ubadhirifu huo umesababisha kampuni hiyo kushindwa kujiendesha ikiwa ni pamoja na kutolipa mishahara ya wafanyakazi kwa muda wa miezi 27 ambayo ni takribani Shilingi Bilioni 3. 7.

Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali itatoa pesa hizo ambazo watalipwa wafanyakazi hao ndani ya kipindi cha wiki Mbili.

Ameyasema hayo mara baada kushuhudia hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli ya MV Viktoria na MV Butiama katika ziwa Viktoria.

Hata hivyo Rais Magufuli amempongeza Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Huduma za Meli nchini Erick Hamisi ambaye ameonyesha muelekeo mzuri wa kuiendeleza kampuni hiyo na kumuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kumpatia nafasi ya Meneja Mkuu na si Kukaimu nafasi hiyo.

Amesisitiza kuwa azma ya serikali ya awamu ya awamu ya Tano ni kuwekeza katika miundombinu mbalimbali yenye manufaa kwa Watanzania wote.

Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kulipa kodi ili serikali iweze kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

De Gea kusaini mkataba mpya na Man United

0

Kipa wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza,- David De Gea anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Kulingana na mkataba huo mpya, De Gea mwenye umri wa miaka 27 na raia wa Hispania atakua akipokea mshahara wa Pauni Laki Tatu na Nusu kwa wiki.

United walimnunua De Gea kutoka Atletico Madrid mwaka 2011 kwa ada ya Pauni milioni 19 na amekua mhimili mkubwa kwa klabu hiyo na mchezaji pekee ambaye kiwango chake hakijawahi kushuka.

Uongozi wa klabu hiyo ya Manchester United umesema kuwa De Gea ni bora tofauti na makipa ambao walitangulia ambao walikua na ulinzi imara huku matokeo yao si ya kuridhisha, wakati De Gea ana ulinzi dhaifu na matokeo mazuri.

FUATILIA MUBASHARA

0

ZIARA YA RAIS Dkt JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI MWANZA AMBAPO RAIS ATASHUHUDIA UWEKAJI SAINI WA MIKATABA YA UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO NA UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA KATIKA ZIWA VICTORIA.

Tufuatilie kwa kupakua TBC Live App Pamoja na website yetu ili kutazama na kusikiliza redio zetu tatu.

(Android) bonyeza????
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.app.tbc

(iPhone) bonyeza??
https://itunes.apple.com/ke/app/tbc-live/id1396199667?mt=8

Website bonyeza

Live Stream

TBC
_Ukweli na Uhakika.

Watanzania waishio China watakiwa kufanya kazi kwa bidii

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania wanaoishi nchini China kufanya kazi kwa bidii na kuchangamkia fursa zilizopo nchini humo.

Akizungumza na Watanzania hao jijini Beijing, Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka kuhakikisha wanazitangaza vema fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

Amesema kuwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi na kufanya shughuli mbalimbali wana nafasi kubwa na muhimu katika kuiletea nchi yao maendeleo.

Waziri Mkuu Majaliwa yuko nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Septemba Tatu mwaka huu jijini Beijing na kufunguliwa na Rais Xi Jinping wa China.

Waziri Mkuu Majaliwa anamuwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo.

Shambulio la kujitoa muhanga lasababisha shule kuporomoka

0

Kumetokea shambulio la kujitoa muhanga katika ofisi moja ya serikali kwenye mji mkuu wa Somalia, – Mogadishu na kusababisha shule iliyokuwa karibu na ofisi hiyo kuporomoka.

Mtu aliyekua kwenye gari amejilipua katika eneo la ofisi hiyo na kusababisha askari watatu kuuawa na watu wengine 14 kujeruhiwa wakiwemo watoto Sita.

Askari hao waliouawa walikua wakijaribu kulizuia gari hilo lililokuwa limejaa milipuko kuingia kwenye ofisi hiyo ya serikali.

Shambulio hilo pia limeharibu nyumba zilizo karibu na ofisi hiyo na kung’oa paa la msikiti mmoja.

Wanamgambo wa Al-Shabab ambaao wamekuwa wakifanya mashambulio mbalimbali kwa zaidi ya miaka 10 nchini Somalia wamedai kuhusika na tukio hilo.

Marekani yafuta msaada wa kijeshi kwa Pakistan

0

Marekani imetangaza kufuta msaada wa Dola Milioni 300 za Kimarekani kwa Pakistan kwa madai kuwa nchi hiyo imeshindwa kuyachukulia hatua makundi ya wanamgambo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Marekani imesema kuwa nchi hiyo itatumia fedha hizo kwa masuala mengine ya dharura.

Marekani imesema kuwa Pakistan imekuwa ikipuuza ama kushindwa kukabiliana na wanamgambo wanaoendesha shughuli zao kwenye ardhi ya nchi hiyo wakiwemo wanamgambo wa Haqqani na wale wa Talibabn.

Mwezi Januari mwaka huu Marekani ilisema kuwa itafuta karibu misaada yote ya shughuli za ulinzi kwa nchi hiyo ya Pakistan.