TRA waonywa kufungia maduka ya wafanyabiashara

0

Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Nchini TRA  kusitisha utaratibu wa kuwafungia wafanyabiashara, biashara zao ili kushinikiza alipe kodi anayodaiwa.

Waziri Mpango amesema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameiagiza TRA  kumfungia biashara mfanyabiashara ambaye ni sugu kwa kukwepa kodi kwa kibali cha Kamishna Mkuu wa Tra.

Aidha ameielekeza TRA kujikita zaidi kutoa elimu kwa mlipa kodi juu ya utunzaji wa vitabu vya hesabu za biashara, na kumpa fursa ya kufanya naye majadiliano kuhusu mpangilio bora wa kulipa malimbikizo ya kodi kwa mkupuo au kwa awamu pamoja na adhabu stahiki kama zilivyobainishwa kwenye Sheria ya Usimamizi wa Kodi 2015.

Rais John Magufuli amjulia hali mama yake anayeugua

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Wasaidizi wake wakimuombea Mama yake Mzazi Bibi. Suzana Magufuli anayepatiwa Matibabu Jijini Dar es Salaam. Desemba 30, 2018.

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu SSRA

0

Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii -SSRA Dkt. Irene Isaka.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA utafanywa baadaye.

Dkt. Irene Isaka atapangiwa kazi nyingine.

TBC kukuletea marudio ya kauli ya Rais Magufuli kuhusu kikokotoo

0

Baada ya taarifa ya Habari ya saa mbili  usiku Televisheni yako ya Taifa -TBC, itakuletea marudio ya kauli ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoitoa mapema leo Ikulu jijini Dar Es Salaam alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Watumishi 13 wa Halmashauri washushwa vyeo Morogoro

0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI Selemani Jafo ameziagiza mamlaka za nidhamu kuwavua nyadhifa zao watumishi 13 wa Halmashauri ya Ulanga kwa kuhusika na wizi na  ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia Tisa.

Waziri Jafo pia ameagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha watumishi wote waliohamishwa kutoka Halmashauri ya Ulanga kwenda Halmashauri nyingine wakiwa na makosa warejeshwe ili kuwezesha vyombo vya dola kufanya kazi yake.

Desemba 27 Mkuu wa mkoa wa Morogoro  Dkt. Kebwe Stephen aliagiza kuitishwa kwa baraza la dharura la Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kujadili taarifa ya Tume iliyoundwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa shilingi Bilioni 2.9 zinazodaiwa kutumika kinyume na utaratibu.

Waziri Mkuu aagiza tathmini ujenzi majengo ya serikali Dodoma

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza mawaziri kukaa na wakandarasi na kutathmini umalizaji wa ujenzi wa majengo ya serikali mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu na kuwataka wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, kutathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na kama wakandarasi hao hawana uwezo wa kumaliza ujenzi  huo wabadilishwe mara moja.

Agizo hilo amelitoa leo alipofanya ziara ya kujionea ujenzi unavyoendelea na kusema endapo wakandarasi hao hawatakuwa na uwezo mkubwa lazima wabadilishwe.

 “Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka na kuipongeza Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote  ni ya Utumishi, ambao katika ujenzi wao ofisi zao uko katika hatua nzuri.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemweleza Waziri Mkuu kwamba kuna wagongaji wa kokoto ambao wamepokea fedha lakini wakaamua kufunga machimbo yao kwa sababu ya sikukuu.

Arusha yapata kiwanda cha kwanza cha kuchakata mazao ya mifugo

0

Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Frank Mwaisumbe amesema kwa mara ya kwanza wilaya hiyo imepata kiwanda cha kuchakata mazao ya mifugo.

Amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuuza tani za nyama elfu kumi kwa siku ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wafugaji kunufaika kwa kuongeza uchumi.

Mwaisumbe amesema kwa sasa jamii ya wafugaji itapata soko la uhakika kupitia kiwanda hicho, hata hivyo  wanahitaji wawekezaji zaidi  ambapo kiwanda kitakuwa na uwezo wakukusanya Bilioni 22 kwa mwaka.

Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yatakiwa kuwa na matumizi mazuri.

0

Rais Dkt. John Magufuli ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na matumizi yanayoridhisha kwa kuwa baadhi ya mifuko imekuwa na matumizi yasiyofaa.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo katika mkutano na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na viongozi wa serikali ambapo amesema mifuko ya hifadhi imekuwa na matumizi yasiyofaa jambo ambalo husababisha mifuko hiyo kuishiwa na kushindwa kufanya kazi kwa malengo yake ya kulipa wastaafu kama inavyotakiwa.

“Kuanzia leo nataka muache kuwa na matumizi ya hovyo ambayo hayana ulazima kwenye mifuko, badala yake mjikite kwenye malengo yaliyokusudiwa”alisema Rais Magufuli.

Ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii -SSRA kuhakikisha inasimamia mifuko hiyo na kuangalia isifanye matumizi yasiyo na tija kwa mifuko.

Rais Magufuli amesema ana mfano wa mfuko wa hifadhi ya jamii unaolipa walinzi wake kiwango kikubwa cha fedha badala ya kutumia walinzi wa SUMA JKT kwa gharama nafuu jambo ambalo lingesaidia kupunguza gharama zisizo za lazima katika mifuko hiyo.

Ameitaka mifuko hiyo kuacha mara moja kufanya uwekezaji usiokuwa na tija kwa miradi ambayo haina faida ambayo badala yake ni upotevu wa fedha huku

uwekezaji huo ukifanyika bila ridhaa ya wanachama jambo ambalo linaleta manung’uniko kwa wanachama wanaochangia.