Mkataba wa ubanguaji wa zao la Korosho wasainiwa

0

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameshuhudia hafla ya utiaji wa saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wamiliki wa kampuni za ndani za kubangua korosho na kutoa wito kwa kampuni zingine kujitokeza na kufanya hivyo.

Waziri Hasunga amesema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuzuia usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi na kuagiza korosho zote zibanguliwe nchini.

Waziri Hasunga amesema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais John magufuli la kuzuia usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi na kuagiza korosho zote zibanguliwe nchini.

Hasunga amesema serikali imepitia vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuanza kuingia makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya ubanguaji wa korosho.

Kampuni ambazo zimesaini mikataba hiyo wamesema baada ya majadiliano ya muda mrefu na serikali wameridhishwa na hatua hiyo na kwamba wataanza ubanguaji kwa wakati.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya kubangua korosho jumla ya Tani 7500 kwa hatua za awali huku ubanguaji huo ukitarajiwa kuanza rasmi Januari 17 mwaka huu ambapo uwezo wa kampuni hizo kubangua korosho kwa mwaka ni Tani Elfu 16 na 400

Viongozi wa Umma wanaotumia madaraka vibaya kushughulikiwa

0


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dakta Mary mwanjelwa  amewaagiza makamishna wa tume ya utumishi wa umma kuanza kuwashughulikia viongozi wanaotumia madaraka vibaya kwa lengo la kurudisha nyuma  sekta ya utumishi wa umma.

Akifungua  mafunzo elekezi kwa makamishna hao wateule Dakta  Mwanjelwa amesema wakati serikali ikiendelea na mkakati  wake wa kuleta mapinduzi ya  uchumi wa viwanda lazima watumishi wa  umma wafahamu kuwa wanahitajika kuwa wabaunifu kiutendaji ili kufikia malengo hayo kwa kuchapa.

Dakta Mwanjelwa pia amewataka makamishna hao kutumia nafasi yao kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya umma  ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za waajiri na wafanyakazi  kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume a Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Dakta Stephen bwana amesema kuwa atahakikisha  matatizo yanayoikabili sekta ya umma yanapatiwa  ufumbuzi wa haraka .

Tume ya Utumishi wa Umma iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais John  Magufuli itakuwa na majukumu ya kushughulikia kero zinazoikabili sekta ya umma .

Mafia washindwa kukagua maendeleo kutokana na ukosefu wa magari

0


Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani inakabiliwa na ukosefu wa magari jambo ambalo linalosababisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na wakuu wa idara kutembea kwa miguu kwenda kukagua  miradi ya maendeleo.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Mohamed Gomvu kwenye  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Pwani kilichofanyika Mjini Kibaha.


Amesema halmashauri yake inakabiliwa na ukosefu wa magari jambo ambalo linasababisha watendaji kushindwa kwenda kusimamia miradi ya maendeleo.

Amesema hivi sasa wilaya nzima ina gari moja tu ambalo linatumiwa na Mkuu wa Wilaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Erick Mapunda amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo amesema pindi inapotokea dharura halmashuri hiyo hulazimika kutumia gari la  kanisa kufanyia shughuli zake.

Akizungumzia tatizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo kushirikiana na afisa anayeshughukia serikali za mitaa kupeleka mara moja suala hilo Ofisi ya Rais Tamisemi ili liweze kushughulikiwa.

Kituo cha mabasi cha Nanenane Dodoma kufanyiwa marekebisho

0


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta Binilith mahenge amemtaka Mkuu wa Wilaya wa Dodoma mjini, Patrobas katambi na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin kunambi kukifanyia maboresho kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Nanenane Jijini Dodoma.

Dokta Mahenge amesema hayo Jijini Dodoma katika ziara yake ya kukagua vituo mbalimbali vya mabasi yaendayo mikoani ambapo ameshuhudia kwa dosari kadhaa katika kituo hicho.

Dokta Binilith Mahenge ilimlazimu kuamka mapema alfajiri na kufika katika kituo kikuu cha mabasi ya abiria waendao mikoani na nchi jirani cha Nanenane ili kushuhudia huduma ya usafirishaji wa abiria na usalama wao.

Amehimiza amehimiza kufanyika ukarabati ambao utaondoa dosori ndogo ndogo alizozishuhudia katika vituo hivyo na kuaagiza wamiliki wa mabasi kuanza kutoa huduma kwa njia ya kieletroniki ili kurahisisha huduma na kuiongezea serikali mapato.

Serikali yatoa onyo kwa wakandarasi watakao hujumu kiwanda cha sukari

0

Waziri Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema serikali haitakuwa na mzaha na wakandarasi watakao bainika kuhujumu mradi wa ujenzi wa kiwanda cha  Sukari cha Mkulazi  kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Waziri Kakunda amesema hayo wilayani kilosa baada ya kutembelea maendeleo ya kiwanda hicho na kusisitiza wakandarasi ambao watapewa zabuni  ya kulima mashamba hayo kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati .

Hapa Waziri Kakunda anaeleza msimamo wa serikali katika kuhakikisha kazi zote zinazoendelea kufanywa katika eneo hilo zinakamilika kwa wakati ili kiwanda hicho kiweze kufunguliwa ifikapo disemba mwaka huu.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba amesema Serikali inaweka mikakati ya  kuhakikisha wakulima wa nje wananufaika kupitia kiwanda hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi  Dokta Elidalita Msita akaeleza changamoto mbalimbali zilizosababisha kusuasua kwa ujenzi huo na mikakati ya kukabiliana nazo.

Kiwanda kipya cha Sukari kujengwa Kilombero

0

Kiwanda cha sukari cha Kilombero  kilichopo mkoani Morogoro kinakusudia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho gharamu kiasi cha shilingi  bilioni 650  ili kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani milioni 1.2 zilizopo sasa hadi kufikia tani  milioni  2.4 kwa mwaka.

Akizungumza katika mkutano wa wadau uliokuwa na lengo la kujadili upanuzi wa kiwanda hicho, Mkurugenzi wa mahusiano wa kiwanda hicho Joseph  Rugaimkamu  amesema ujenzi wa kiwanda hicho kipya utaenda sambamba na upanuzi wa mshamba ya miwa ya kiwanda pamoja na wakulima wan je  ili kukidhi mahitaji ya sukari katika soko la ndani na nje ya nchi.

Amesema ujenzi wa kiwanda hicho  utasaidia kuongeza upatikanaji wa sukari katika soko la ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dakta  Stephen Kebwe amezitaka halmashauri za Kilosa na Kilombero kushiriki kikamilifu ili kufanikisha mchakato wa  utekelezaji wa maagizo ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha sukari iliyopo nchini inajitosheleza .

Serikali yaombwa kutoa muda wa kutumika sheria mpya ya uzito wa malori

0

Chama cha Wasafirishaji Tanzania kimeiomba serikali kuongeza muda zaidi wa kuanza kutumika sheria mpya ya uzito wa malori ya Afrika Mashariki iliyoanza Januari Mosi mwaka huu ili kumaliza changamoto zinazojitokeza ikiwemo kukwama kwa magari katika mpaka wa Tunduma.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania Omary Kiponza amesema sheria hiyo inakinzana na ile ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Sadc kwani tayari kuna mizigo iliyopakiwa kuja Tanzania imekwama mpakani na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara na kuathiri uchumi wa bandari za Tanzania.

Akijibu hoja hizo kwa njia ya simu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema walitoa muda wa miezi sita kwa wadau wa usafirishaji kupitia sheria hiyo kabla ya kuanza utekelezaji wake..

Sheria ya uzito wa malori ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanza kutumika Januari Mosi mwaka huu lengo likiwa ni kulinda miundombinu ya barabara.

Simona ashindwa kumfunga Barty katika mchezo wa tenes

0

Mchezaji namba moja kwa ubora wa tesniss duniani kwa upande wa kinadada  Simona Halep  ameshindwa kutamba mbele ya   Ashleigh Barty wa Australia katika michuano ya  Kimataifa ya Sydney.

Mromania huyo ambaye alikuwa nje ya mchezo huo kwa takribani miezi mitatu kutokana na kuwa majeruhi amenyukwa seti mbili kwa bila kwa matokeo ya seti  6-4 na  6-4 na Barty ambaye ni mchezaji namba 15 kwa ubora duniani.

Halep mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni bingwa wa mashindano ya wazi ya Ufaransa, ameanza mashindano hayo bila ya kocha wake huku pia akitarajia kushiriki mashindano makubwa ya teniss ya wazi ya Australia hivi karibuni.