Rais Magufuli ataka uwekezaji wenye tija

0

Rais Dkt. John Magufuli amesema anataka uwekezaji utakaofanyika nchini uwe wenye tija kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika hafla ya utiaji saini wa mkataba mpya baina ya Kampuni ya Bharti Airtel  na serikali ya Tanzania.

Amesema kuanzia sasa lazima uwekezaji wote uwe na faida na tija na  kama nchi iweze kufaidika  na si kupata hasara.

“Nataka uwekezaji wenye tija na malengo hapa nchini  na si kuingia mikataba yenye kuleta hasara” alisema Rais Magufuli.

Tanzania na Kampuni ya Bharti Airtel zimekubaliana makubaliano mapya ambapo kwa sasa Tanzania itakuwa na umiliki wa hisa 49 kutoka hisa 40 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9 na Kampuni ya Bharti Airtel ikibakiwa na hisa asilimia 51 tofauti na awali ilivyokuwa ikimiliki asilimia 60 ya hisa

Bodi ya Mikopo yaweka mazingira mazuri kwa wadaiwa sugu.

0


Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wadaiwa wa bodi hiyo ambayo hadi sasa inadai shilingi Bilioni 291 kwa wadaiwa sugu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Abdul Razaq Badru amesema katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 Bodi ya mikopo imekusanya jumla ya shilingi bilioni 94 na kuvuka lengo la kukusanya bilioni 71 katika kipindi hicho.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari bodi ya mikopo imetangaza rasmi kujiunga na mfumo wa serikali wa ukusanyaji mapato yaani (Government e-payment Gateway – GEPG) na kusisitiza kuwa malipo yote kwenda bodi ya mikopo yatapokelewa kwa mfumo unaofuatwa na taasisi za serikali.

Rais wa zamani wa Ivory Coast aachiwa huru

0

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai Icc imemuachilia huru aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

Majaji wa mahakama hiyo wamesema hana kesi ya kujibu kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha makosa dhidi yake na kuamrisha kuachiwa huru mara moja.

Gbagbo alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya raia wa Ivory Coast kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliokuwa na mzozo wa 2010 zilizopelekea takriban watu 3000 kuuwawa na wengine 500,000 kuachwa bila makazi .

Gbagbo alikamatwa  mwaka 2011 na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa Un pamoja na wale wanaoungwa mkono na UfaransA waliokuwa wakimuunga mkono mpianzani wake Alassane OuattarA.

Wafuasi wa Gbagbo wameonekana wakisherehekea katika maeneo mbalimbali  kufuatia kuachiwa huru kwa kiongozi huyo.

Serikali yaongezewa hisa umiliki Kampuni ya simu Airtel

0

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Bharti Airtel leo zimetiliana saini makubaliano na uongezwaji wa umiliki wa hisa za serikali kutoka asilimia 40 hadi 49 na Airtel kubakia na hisa 51 kutoka hisa 60 za awali.

Akizungumza baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo Ikulu jijini Dar Es Salaam, Rais Dkt. John Magufuli amesema ongezeko hilo la hisa ni tija kubwa kwa taifa na kufanya uwekezaji wenye faida.

Amesema tangu kuanza kwa kampuni hiyo miaka tisa iliyopita hapa nchini Tanzania haijawahi kufaidika na gawio lolote na kwamba sasa makubaliano yamefikiwa.

Pia mbali na makubaliano ya uongezwaji wa hisa pia Tanzania itapatiwa  shilingi Bilioni moja kila mwezi kwa muda wa miaka mitano kama fidia kutokana na serikali kutopata gawio lolote.

“Hii ni hatua nzuri kwa nchi kwani italenga kuleta wawekezaji wenye nia njema ya kuleta maendeleo kwa nchi ‘alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema makubalino hayo kufikiwa haikuwa rahisi ambapo ameipongeza kamati ya upande wa serikali iliyokuwa ikiongozwa na Waziri wa  Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi aliyeongoza majadiliano na wawakilishi wa Kampuni ya Bharti Airtel mpaka kufikiwa kwa makubaliano hayo.

Katika makubaliano hayo suala la uongozi serikali itapendekeza Mkurugenzi Mkuu upande wa ufundi ambaye ataajiriwa na Kampuni ya Bharti Airtel kama makubaliano yanavyotaka kuwa katika uongozi wa kampuni hiyo kwamba serikali ya Tanzania itakuwa na kiongozi katika upande wa ufundi na Bharti Airtel wao watabaki na nafasi ya Mtendaji Mkuu na Mtendaji kwenye masuala ya fedha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Bharti Airtel, Sunil Mittal ameshukuru kwa kampuni yake kufikia makubaliano hayo na serikali ya Tanzania kwani watahakikisha wanaendeleza uhusiano mzuri kwa makubaliano waliyofikia.

Mwenyekiti huyo ametoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.3  kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii ambapo Rais Magufuli ametoa agizo kuwa fedha hizo zitakwenda kuongezwa katika Hospitali inayojengwa jijini Dodoma.

Manchester City yapata ushindi dhidi ya Wolverhampton Wenderres

0

Ligi kuu ya England imeendelea hapo Jumatatu Januari 14  ambapo bingwa mtetezi MancManchester City yapata ushindi dhidi ya Wolverhampton Wenderreshester City inazidi kuifukuza kwa kasi Liverpool katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu .

Manchester city iliifunga timu ya  Wolverhampton Wenderres mabao matatu kwa bila kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa a la Etihad.

Mabao mawili ya Gabriel Hesus katika daika ya 10 na 39 na bao lingine la  kujifunga la Conor Coady katika dakika ya 78 yakafikisha idadi ya mabao matatu .

Kwa matokeo hayo Manchester City imefikisha alama 53 kwenye msimamo wa ligi  kuu ya England ikiwa ni tofauti ya alama nne na vinara Liverpool wenye alama 57.