Al Shabaab wadai wamelipiza kisasi shambulio nchini Kenya

0

Wapiganaji wa kikundi cha Al Shabaab cha nchini Somalia wanadai kuwa shambulio la kigaidi walilotekeleza mjini Nairobi, mwishoni mwa wiki ilikuwa ni hatua ya kulipiza kisasi kwa serikali ya Israel.

Wapiganaji hao wanasema wamekasirishwa na hatua ya serikali ya Israel kuhamishia mji wake mkuu mjini Jerusalem, kutoka mjini Tel Aviv, mji unaothaminiwa na mataifa ya Palestina na Israel.

Rais Magufuli azungumza na Rais wa zamani wa Nigeria

0


Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Dkt. Olusegun Obasanjo Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Dkt. Obasanjo amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika uongozi wake ikiwemo kupambana na rushwa, kuimarisha utoaji wa elimu, kuimarisha miundombinu, kuongeza nishati ya umeme, kuboresha usafiri wa ardhini na angani na jinsi wadau wa ndani na nje wanavyopaswa kuelewa juhudi zinazofanyika.

Dkt. Obasanjo amesema Rais Magufuli amedhihirisha kuwa kiongozi imara wa kusimamia mambo muhimu yenye maslahi kwa nchi yake na amebainisha kuwa licha ya kwamba maendeleo ya nchi hayapatikani mara moja lakini kwa muda mfupi Rais Magufuli amefanya juhudi za kuimarisha maeneo ya huduma za kijamii, kukiimarisha chama chake cha siasa (Chama Cha Mapinduzi – CCM) na kwamba ameonesha kuwa anakijua anachokifanya katika maeneo ya uchumi.

“Tusijisahau kwamba ukoloni mamboleo bado upo na mabeberu bado wanaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha wanatunyonya, na kiongozi yeyote wa Afrika anayethubutu kuwazui hawezi kuwa rafiki wa hao ambao walikuwa wakinufaika kwa kutunyonya” amesisitiza Dkt. Obasanjo.

Chaneli ya Utalii yatakiwa kuonekana ndani na nje ya nchi

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa kamati ya uboreshaji na undelezaji wa chaneli mpya utalii ya Tanzania Safari kuweka jitihada za uwekezaji kwa kusambaza huduma ya chaneli hiyo katika visimbusi mbalimbali ili kupanua wigo wa kuonekana ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo Jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya maendeleo  ya chaneli hiyo ilipofikia tangu kunzishwa kwake.

Kamati ya  uboreshaji na undelezaji wa chaneli hiyo imewasilisha taarifa ya maendeleo  .

 Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza kamati hiyo na kutoa wito wa kupanua wigo wa chaneli hiyo katika uwekezaji.

Pia ameitaka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuingiza bajeti kwa ajili ya Tbc kuweza kuendesha chaneli hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tbc  Dokta  Ayub Rioba amesema kupitia chaneli hiyo watanzania watajua vivutio vilivyopo na kuvutunza .

Hali ya kawaida yarejea Nairobi

0

Umoja wa Afrika -AU na Umoja wa Mataifa – UN wamelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea katika hoteli ya Dusit mjini Nairobi nchini Kenya, Jumanne Januari 15 na kutuma salamu za pole kwa waliofiwa na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema shambulio hilo linakumbusha umuhimu wa kudhibiti ugaidi barani Afrika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani hilo na kusema yuko pamoja na watu wa Kenya na serikali yao.

Katika hatua nyingine Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuwa watu wote waliohusika na shambulio la kigaidi katika hoteli ya Dusit mjini Nairobi na kuwashikilia watu kadhaa mateka kwa saa 20 wameuawa na hali ya utulivu imerejea nchini humo.

Kenyatta amelihutubia taifa hilo leo asubuhi na kutangaza kuwa watu kumi na wanne wamekufa, baada ya watu hao wenye silaha kushambulia hoteli hiyo na kuanza kufyatua risasi. Watu zaidi ya mia saba waliokuwa katika eneo hilo la hoteli wameokolewa.

Viongozi wa upinzani nchini Kenya wamewasifu maafisa usalama nchini humo waliofanya juhudi kuwadhibiti watu hao wenye silaha na kuweza kulidhibiti tukio hilo kwa haraka.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema washambuliaji hawakuangalia tabaka, bali shambulio lao lililenga kila mtu hivyo ni vema wananchi wa Kenya kuungana ili kupambana na vitendo vya ugaidi.

Makamanda watatu wa polisi wavuliwa vyeo

0

Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amewavua madaraka makamamanda wa polisi wa watatu kwa tuhuma za kutotekeleza maagizo ya viongozi na kuamuagiza katibu mkuu  wizara ya  hiyo kuunda tume itayochunguza tuhuma za vitendo na mianya ya rushwa katika jeshi hilo husuusani katika kikosi cha usalama barabarani ili kuchukua hatua.

Waziri Kangi Lugola ametoa uamuzi huo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari sambamba na kumtaka kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kujitathmini kama anafaa kuendelea na nafasi hiyo akianza na suala la tume.

Makamanda hao ni pamoja na Salum Hamduni (Ilala),Emmanuel  Lukula (Temeke) na Ramadhan Ngazi(Arusha).

Waziri amesema pia makamanda hao wa polisi wa mikoa mitatu wamekuwa wakishindwa kufanya majukumu na maagizo ya serikali katika utendaji wao.

Pi waziri Lugola amepiga marufuku kwa kikosi cha usalama barabarani kubambikiza makosa mengi kwa madereva na kutoza faini katika makosa hayo kinyume na sheria ya usalama barabani.

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za mabalozi

0

Rais Dkt John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi kutoka nchi tatu ikiwemo Brazili,Korea Kusini  na Malawi.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu- Dar es salaam Rais Magufuli  amemuomba Balozi wa Brazil hapa nchini Antonio  Agusto Martin Siza kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Brazil kwa kushirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Balozi wa Brazil nchini Tanzania  atawakilisha nchi yake kwa kipindi cha miaka mitatu balozi wa amesema nchi yake ipo tayari kushirikiana katika biashara,uendelezaji wa mradi wa kilimo cha pamba, kuwasaidia watu wenye seli mundu, na kuboresha miundombinu.

Wanawake waaswa kutokubali rushwa ya Ngono ili kupata ajira

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa amewataka wanawake kuacha kutumika kwa lengo la kupata vyeo ama kazi katika taasisi zozote nchini.

Naibu Waziri Mwanjelwa ameyasema hayo katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Tbc ambapo amesema mwanamke ni hekalu takatifu na si mashine ya kumfurahisha mtu mwingine bila makubaliano.

Amesema mwanamke yeyote anayefanyiwa hivyo ahakikishe anaripoti suala hili katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa hatua zaidi.

Nidhamu ya watumishi wa Umma yaongezeka

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa amesema nidhamu na heshima kwa utumishi wa umma kwa sasa imerejea kwa kiwango kikubwa .

Dokta Mwanjelwa amesema hayo katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Tbc ambapo amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa umma wamekuwa na nidhamu jambo ambalo linasaidia katika ofisi nyingi za umma kufikia malengo husika.

Naibu Waziri Mwanjelwa amesema nidhamu imerejea sana katika utumishi wa umma na kuwaomba watumishi wa umma kuendeleza nidhamu hiyo zaidi kwani inajenga taswira nzuri kwa nchi.

Amewataka watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa na kuweza kufikia malengo muhimu.