Wachezaji wa timu ya Zesco United ya nchini Zambia, tayari wamewasili nchini kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Yanga, mchezo utakaochezwa Keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kutangazwa moja kwa moja na TBC Taifa kuanzia saa Kumi alasiri.