Yanga yaifumua Iringa United 4 bila

0
478

YANGA imeingia Hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Iringa United jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam

Papy Kabamba Tshishimbi aliifungia Yanga bao la kwanza dakika ya nane akimalizia krosi ya mzawa, kiungo Deus David Kaseke

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana naye akafunga bao la pili dakika ya 10 akimalizia mpira uliowapita mabeki wa Iringa United baada ya krosi ya beki wa kulia, mzawa Cleophas Sospeter Mkandala

Beki Mghana Lamine Moro akafunga bao la tatu kwa kichwa dakika ya 39 akimalizia kona maridad ya Sibomana ambaye pia alimpasia Mkongo mwingine, mshambauliaji David Molinga Ndama ‘Falcao’ kufunga bao la nne dakika ya 70.