Yanga wainyuka Tanzania Prisons moja bila majibu

0
404

Klabu ya soka ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi kuu soka ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Ushindi huo, unawafanya Yanga kufikisha pointi 21 katika michezo 10 wakizidiwa pointi tatu na Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili, ikiwa na michezo mitatu zaidi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wakiwa kileleni na alama 28 baada ya kucheza michezo 11

Bao pekee la Yanga hii leo limefungwa na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana dakika ya tano ya mchezo akimalizia mpira wa kurushwa kutoka kwa kiungo Mzanzibari, Abdulaziz ‘Bui’ Makame kutoka upande wa kulia.