Yanga SC yatinga fainali ya ASFC

0
211

Yanga SC imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuifunga Simba SC katika mchezo wa nusu fainali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Goli pekee lililoipeleka Yanga fainali limefungwa na Feisal Salum dakika ya 26, na kutosha kupeleka kilio msimbazi.

Yanga sasa inamsubiri mshindi wa mchezo wa pili wa nusu fainali utakaopigwa Mei 29 mwaka huu katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kati ya Azam FC na Coastal Union.

Msimu huu yanga imejiweka katika nafasi nzuri ambapo sasa ipo nyuma alama tatu kuelekea kutwaa ubingwa wa NBC na sasa imetinga fainali ya ASFC.