Yanga kumaliza ukame wa makombe

0
1073

Timu ya Yanga imesema inaamini umoja na mshikamano ndani ya timu hiyo ndio silaha kubwa ya kuchukua kikombe cha ligi msimu huu baada ya kukosa kwa misimu minne mfululizo.

Hayo yamesemwa na Haji Manara mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya timu hiyo ambapo amewashukuru viongozi, benchi la ufundi na mashabiki baada ya kutwaa kombe la ngao ya jamii iliyochezwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Manara ameipongeza TFF kwa maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku akitoa wito kwa waamuzi kufuata sheria na kanuni za soka kikamilifu.

“Kwa sasa tuna waamuzi wazuri na tunaamini watafanya vizuri, ila wajitahidi kuepuka makosa ambayo yanawesa kuleta shida kwenye ligi yetu,” amesema Manara.

Aidha, imewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa kitu kimoja na kuombea dua timu yao kipindi hiki chote cha msimu wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo tayari imesafiri kuelekea Kagera katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa Jumatano hii na kutangazwa mbashara TBC Taifa na TBCOnline (YouTube).