Yanga bingwa ngao ya Jamii

0
1870

Klabu ya soka ya Yanga imeibuka bingwa wa ngao ya jamii baada ya kuifunga Klabu ya soka Simba bao 1-0.

Bao lililo amua mchezo huo limefungwa dakika ya 12 na mchezaji wa kimataifa wa yanga Fiston Mayele.

Mpaka mchezo huo unaenda mapumziko Yanga ilikua mbele kwa bao hilo moja kwa bila.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko lakini hayakubadilisha matokeo ya mchezo huo.

Mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi Ramadhani Kayoko inapulizwa Yanga ikaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Kwa ushindi huo Yanga huo inakua bingwa kwa mara ya sita ikilingana na watani wao Simba.