Wydad mabingwa wapya Afrika

0
255

Miamba ya Soka ya nchini Morocco Wydad Casablanca wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Klabu bingwa Afrika, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi National Al Ahly ya Misri mabao 2 – 0.

Magoli ya dakika ya 15 na 48 yaliyofungwa na Zouhair El Moutaraji yameifanya Wydad kutwaa taji lake la 3 la michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Al Ahly waliokuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo lakini wameshindwa kufurukuta katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco

Ubingwa huo wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh. Bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh. Bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili

Kwa ushindi huo ni wazi kuwa Klabu za Soka za nchini Morocco zimetawala Soka la Afrika msimu huu baada ya RS Berkane kutwaa taji la kombe la Shirikisho barani Afrika majuma mawili yaliyopita.