Wizards yaibwagiza Lakers

0
1232

Timu ya Los Angeles Lakers imefungwa kwa alama 128 kwa 110 na Washington Wizards katika ligi Kuu ya Kulipwa ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA.
Katika mchezo huo, mchezaji John Wall ameibuka shujaa kwa kufunga alama 40 zilizochangia ushindi huo wa Wizards.

Pamoja na wachezaji Lebron James na Kentavious Cald (Well Pope) kwa pamoja kupambana na kufunga alama 38, bado hazikutosha kuiokoa timu yao ya Lakers na kipigo hicho kutoka kwa Washington Wizards.

Katika dimba la Quicken Loans mjini Cleveland – Ohio, wenyeji Cleveland Cavaliers wamepokea kipigo cha 23 kwa msimu huu baada ya kunyukwa alama 128 kwa 105 na timu ya Philadelphia 76’ERS waliokuwa wakiongozwa na mchezaji Joel Embird aliyefunga alama 24.

Nayo timu ya Pecers imeinyoosha New York Knicks kwa kuitandika alama 110 kwa 99.