Watatu wakamatwa sakata la ubaguzi wa rangi kwa Vinicius Jr

0
209
Soccer Football - LaLiga - Valencia v Real Madrid - Mestalla, Valencia, Spain - May 21, 2023 Real Madrid's Vinicius Junior gestures towards a fan REUTERS/Pablo Morano

Matusi na ubaguzi wa rangi ulioelekezwa kwa mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Jr, vimechochea mjadala mkali kuhusu ubaguzi wa rangi katika michezo na ikiwa jamii ya Kihispania ina tatizo na suala hilo.

Polisi nchini Hispania wamekamata watu watatu kuhusiana na unyanyasaji wa kibaguzi dhidi ya Vinicius Jr, ambaye alikabiliana na mashabiki wa Valencia katika uwanja wa Mestalla, ambao alidai kuwa walimtolea kelele za kibaguzi.

Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alisema ligi ya soka ya Hispania “inamilikiwa na watu wenye ubaguzi.”

Baada ya tukio hilo, Rais wa Brazil, Luiz InĂ¡cio Lula da Silva, alionya dhidi ya kuacha vitendo vya ubaguzi wa rangi kutawala katika viwanja vya mpira, na serikali yake ilitoa taarifa ikisema inasikitika sana kutokana na kutokuwepo kwa hatua za kushughulikia tatizo hilo na mamlaka za Kihispania.

Tukio limevuka mipaka ya Hispania jijini Rio de Janeiro taa zinazomulika sanamu ya Yesu zimefifia kama ishara ya mshikamano na mchezaji huyo.

Rais wa La Liga, Javier Tebas, amekanusha vikali madai yaliyotolewa akisema “Hispania wala La Liga hawana ubaguzi wa rangi, ni jambo lisilofaa kusema hivyo.”