Simba yaingia Mkataba wa Bilioni 2 na Vunja Bei

0
158

Kampuni ya Vunja Bei inayoongozwa na Fred Ngajiro maarufu(Fred Vunja bei) imeshinda tenda ya kusambaza na kutengeneza jezi na vifaa vya michezo vya Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, – Barbara Gonzalez amewaambia Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuwa kampuni ya Vunja Bei itafanya kazi hiyo kwa mkataba wa miaka miwili ambao una thamani ya shilingi bilioni mbili.

Amesema kampuni hiyo ya Vunja Bei imeshinda tenda hiyo baada ya kushindanishwa na kampuni nyingine 11 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mchakato wa kupata mzabuni kwa ajili ya kusambaza na kutengeneza jezi pamoja na vifaa vya michezo vya Klabu ya Simba ulianza mwezi Desemba mwaka 2020.