Vipers SC imetangaza kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Beto Bianchi mara moja baada ya miezi miwili kibaruani.
Klabu hiyo ya Uganda imemshukuru Bianchi kwa juhudi zake za kutochoka wakati akiwa klabuni hapo na kumtakia mafanikio aendako.
Kocha huyo kutoka Brazil alitambulishwa Januari 10 mwaka huu akichukua nafasi ya Roberto Oliviera ambaye alijiunga Simba SC ya Tanzania.
Vipers imekuwa na mwenendo mbaya katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika michezo minne, imefungwa mitatu na kutoka suluhu mmoja.