Utalii wa Baiskeli Mlima Kilimanjaro

0
315

Watanzania walioungana na waendesha baiskeli duniani akiwemo mwendesha baiskeli nguli kutoka Uingereza Hannah Barnes wametembea kilomita 275 kupitia Mlima Kilimanjaro hadi Ziwa Natron kwa muda wa siku nne ili kuutangaza Utalii wa baiskeli katika mlima Kilimanjaro

Akizungumza mara baada ya kumaliza safari hiyo Miss Utalii Njombe 2020 Zawadi Mwambi amesema kwake imekuwa ni faraja kuendelea kushirikiana na waendesha baiskeli duniani katika kuutangaza utalii wetu hasa Mlima Kilimanjaro ambao kwa miaka mingi wengi wamekuwa wakipotoshwa na sehemu mlima huo ulipo

Kwa Upande wake Mwendesha baiskeli kutoka Uingereza Hannah Barnes amesema amevutiwa sana na hali ya hewa ya mlima kilimanjaro na imekuwa ni rafiki kwa waendesha baiskeli kumaliza safari yao salama

Waendesha baiskeli kutoka Tanzania wamekuwa mstari wa mbele katika kuendelea kuvitangaza vivutio kwa utalii nchini wakiwa katika misafara yao mikubwa kama vile Twende Butiama safari ambayo inawachukua siku 10 kutembea kilomita 1500 kutoka Dar es Salaam hadi Mwitongo Butiama