Mchezo wa Ligi Kuu England Dabi ya Manchester umemalizika kwa wenyeji wa mchezo huo Manchester United kuing’arisha Manchester kwa rangi nyekundu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa bila dhidi ya Manchester City
Mabao ya United yamefungwa na Martial dakika ya 30 huku bao la 2 likifungwa na McTominay dakika ya 90 ya mchezo huo
Kwa matokeo hayo Manchester United wanaongeza alama 3 na kufikisha alama 45 katika nafasi ya 5 wakiendelea kupigania nafasi nne za juu huku Manchester city yenyewe ikibaki na alama 57 katika nafasi ya pili na kufanya mambo kuzidi kuwa mepesi kwa Liverpool ambao ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 82 hivyo kuwazidi Manchester city kwa alama 25
Katika mchezo wa awali Chelsea imeitandika Everton mabao 4 kwa nunge na kuongeza alama 3 muhimu ikifikisha point 48 katika nafasi ya 4