Twaha Kiduku amchapa Mwarabu

0
189

Bondia Twaha Kiduku, ameendeleza ubabe wake baada ya kumchapa kwa alama za majaji wote watatu (Unanimous Decision) bondia Abdou Khaleed kutoka Misri.

Kwa ushindi huo wa pambano hilo la raundi 10 lililopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, Kiduku ameutetea ubingwa wake wa mabara wa UBO uzani wa Super Middle.

Hili ni pambano la 20 kushinda kwa Kiduku, akitoka sare 1 na kupoteza 8, sasa akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 29.