TUNAENDA COSAFA KUSHINDA SIO KUSHIRIKI- KOCHA WA TANZANITE

0
236

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ Bakari Shime amesema kuwa wanakwenda Afrika ya Kusini kupeperusha vema Bendera ya Taifa kwenye michuano ya COSAFA inayotarajiwa kufanyika August Mosi mwaka huu.

Tanzanite wameondoka leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya COSOFA inayotarajiwa kuanza Agosti mosi mpaka 11 baada ya kualikwa na shirikisho la vyama vya soka kusini mwa Afrika ambapo Jumla ya wachezaji 20 wameondoka katika msafara huo.

Shime amesema wanakwenda na wachezaji hao baada ya kuwaona kambini na kila mmoja amechaguliwa kulingana na uwezo wake wa kusakata soka katika nafasi walizochaguliwa kucheza.


Kocha huyo amewataka Watanzania kuwa na imani ya timu yao kwani wanakwenda  kufanya kazi kwa ajili ya Taifa.