TRA yavunja rekodi ya mapato

0
120

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya shilingi trilioni 12.46 katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023, huku makusanyo ya Desemba 2022 (TZS trilioni 2.76) yakivunja rekodi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwaka 1996.

Makusanyo ya nusu ya kwanza ni sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya shilingi trilioni 12.48.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRA na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la shilingi trilioni1.35 ikilinganishwa na shilingi trilioni 11.11 iliyokusanywa katika kipindi kama hicho Mwaka wa Fedha 2021/22.