Wachezaji 25 ambao ni sehemu ya watu 38 wanaounda timu ya TP Mazembe ipo njiani kuelekea Dar es Salaam, Tanzania ikitokea Lubumbashi, DR Congo.
Miamba hiyo ya DRC itakuwa wageni wa Yanga SC katika mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumapili, Februari 19, 2023 katika Uwanja wa Bejamin Mkapa.
Wakati TP Mazembe ikitafuta ushindi wa pili ili kufikisha alama sita, Yanga itashuka dimbani ikitafuta ushindi wa kwanza baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0 katika mchezo wa kwanza.
Mchezo huo utarejesha kumbukizi za Agosti 2016 ambapo timu hizi zilikutana kwenye hatua kama hii, TP Mazembe ikiondoka na ushindi wa magoli 3-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stade TP Mazembe.
Magoli katika mchezo huo yalifungwa na na Jonathani Bolingi dakika ya 28, Raiford Kalaba dakika ya 55 na 64, huku goli ka kufutia machozi la Yanga likifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 75.